Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Hamisa H. Kalombola na Makamishna wa Tume leo tarehe 14/08/2023 wameanza ziara ya siku tatu kutembelea Zanzibar ambapo wanatarajia kukutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, Ofisini kwake Mazizini. Katika ziara hii Makamishna wa Tume watatembelea pia Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar, Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar na Tume ya Utumishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Mwenyekiti wa Tume katika ziara hii atakuwa na Makamishna, Mhe. Khadija A.M. Mbarak, Mhe. Balozi John M. Haule. Mhe. Immaculate P. Ngwale, Mhe. Balozi Adadi M. Rajabu, Mhe. Susan P. Mlawi na Mhe. Nassor N. Mnambila pamoja na Bw. Mathew M. Kirama, Katibu wa Tume.
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.