Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

MHE.HAMISA KALOMBORA (JAJI MSTAAFU) AMEFUNGA MAFUNZO KATI YA TUME NA WASHIRIKI KUTOKA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA, KANDA YA ZIWA

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji mstaafu Mhe. Hamisa Kalombola amefunga mafunzo yaliyoandaliwa na Tume kwa washiriki kutoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, waliopo katika Kanda ya Ziwa na yamefanyika katika ukumbi wa Rocky City Mall, Jijini Mwanza.

Mhe. Kalombola amewasisitiza watumishi wa umma kusoma na kuelewa  Marekebisho ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022, muhimu zaidi  Kanuni ya 61(4) inayohusu Tume kuanza kutoa uamuzi kwa kutumia vielelezo vya upande mmoja. 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.