Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
Jaji Mst. Mhe. Hamisa H. Kambola, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma amekutana Ofisini kwake Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Khadija Shamte Mzee aliyeitembelea Tume kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia jmasuala ya Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Bw. Mathew M. Kirama, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw, Mussa Kombo Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.