Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Rais Samia Suluhu Hassan, "Idadi ya Watu Tanzania imefikia 61,741,120"

Rais Samia Suluhu Hassan amesema idadi ya watu Tanzania imefikia 61,741,120 na katika idadi hiyo, Tanzania Bara ni 59,851,357 na Zanzibar ina watu 1,889,773. Aidha, amesema Wanawake ni 31,687,990 sawa na asilimia 51 ya Watanzania wote na Wanaume ni 30,530,130 sawa na asilimia 49 ya Watanzania. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza matokeo ya Sensa ya idadi ya watu, majengo na anuani za makazi yaanze kutumika kupanga miradi ya Wananchi. Mheshimiwa Rais amezinduamatokeo haya ya mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 na Mwongozo wa Kitaifa wa matumizi ya matokeo hayo. Rais Samia amesema Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi umeandaliwa ili kuhakikisha matokeo hayo yanatumika kutunga, kutekeleza Sera na Mipango ya Maendeleo ya Kisekta katika ngazi zote za Utawala.  Idadi ya watu nchini imeongezeka kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na Sensa iliyotangulia ya mwaka 2012 ambayo idadi ya Watu ilikuwa 44,928,923.

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

31-05-2022

TAARIFA KWA UMMA

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.