Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA (1961-2021)

Baada ya Uhuru mwaka 1961, Utumishi katika Sekta ya Umma  katika Nyanja mbalimbali ulishikiliwa na wageni. Hivi sasa, tunapoadhimisha miaka 60 baada ya Uhuru hali imebadilika sana ambapo Utumishi wa Umma sasa unaendeshwa na Watanzania wenyewe katika Nyanja zote ambapo kupitia juhudi zilizofanyika katika awamu zote za Uongozi wa Nchi hii, wataalam katika fani mbalimbali wameandaliwa wakijumuisha Wahandisi, Makandarasi, Walimu  na Madaktari wenye sifa na wanaofanya kazi kwa weledi.
Kupitia programu mbalimbali za kuelimisha na kuhamasisha utendaji wenye matokeo kwa watumishi wa umma, Tume imeendelea kutoa wito kwa watumishi wa umma kuheshimu Sheria, kufanya kazi kwa Weledi, Uadilifu na Uzalendo ili kuwezesha Utumishi wa Umma kuwa daraja muhimu la uhusiano mzuri kati ya Serikali na Wananchi wake. Kwa kufanya hivyo, Kauli Mbiu ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya “Kazi iendelee” itakuwa imetekelezwa kwa vitendo.


 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.