Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

MUHOJI AFUNGUA KIKAO KAZI KATI YA TUME NA WADAU KUJADILI MPANGO MKAKATI WA MWAKA 2021/22 – 2025/26

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji leo amefungua Kikao Kazi kinachofanyika Mkoani Morogoro kati ya Tume na Wadau kujadili Mpango Mkakati mpya wa Tume wa mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026 ulioandaliwa baada ya kuhuisha Mpango Mkakati uliokuwepo awali wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21.

Muhoji amesema kuwa majukumu yaliyo kasimiwa kwa Tume ya Utumishi wa Umma ndiyo yanaipa Tume uhalali wa kuwa na Mpango Mkakati huu ulioandaliwa. Amewakumbusha washiriki kuwa kazi kubwa ya Tume ni kuhakikisha kwamba katika Utumishi wa Umma panakuwepo na Uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia uendeshaji wa masuala ya Rasilimali Watu.

 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.