Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

HAFLA YA KUWAAGA WASTAAFU WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA-02 JULAI 2021

Katibu Mkuu Ikulu, Dkt. Moses M. Kusiluka amemwakilisha Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa Balozi Hussein Kattanga, katika hafla ya kuwaaga Wastaafu Viongozi (2) wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji (Katibu wa Tume) na Bw. Bambumbile Mwakyanjala (Mkurugenzi wa Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti). Hafla hii ilihudhuriwa pia na Makamishna wa Tume wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana, Bw. Cosmas Ngangaji (Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI) aliyemwakilisha Katibu Mkuu UTUMISHI pamoja na wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Umma. Hafla hii imefanyika 02 Julai, 2021 katika Ukumbi wa Mkutano wa HAZINA, Jijini Dar es Salaam..

   

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.