Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

"OPRAS" NI MOJA YA ENEO LENYE CHANGAMOTO - MUHOJI

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji amesema “OPRAS” ni moja ya eneo lenye changamoto katika Kaguzi za Rasilimali Watu zinazoendeshwa na Tume ya Utumishi wa Umma. Bwana Muhoji amesema haya hivi karibuni Mkoani Kilimanjaro wakati akifunga mafunzo kwa watumishi wa KADCO yaliyoendeshwa na Tume.
“Moja ya eneo linaloonesha kuwa na changamoto katika kaguzi za Rasilimali Watu zinazoendeshwa na Tume ya Utumishi wa Umma ni eneo la OPRAS. Nimefarijika sana kuona kuwa pamoja na maeneo mengine, mmepata fursa ya kuelekezwa namna ya kujaza na kutekeleza OPRAS kwa mujibu wa sheria. Ni matarajio yangu kuwa baada ya mafunzo haya, sasa mtajaza OPRAS kwa kuzingatia vipindi vya ujazaji na kuwa na malengo ya utendaji kazi yaliyo “SMART” ili utendaji kazi wenu utathminiwe kiusahihi zaidi kwa lengo la kufikia malengo ya mtumishi mmoja mmoja pamoja na ya Taasisi kwa ujumla” alisema.  

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.