Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

KAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA MHESHIMIWA GEORGE YAMBESI , AMEFUNGUA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA KADCO-KILIMANJARO LEO TAREHE 10 MEI 2021

Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa George Yambesi, leo tarehe 10 Mei, 2021 amefungua mafunzo yanayotolewa na Tume kwa watumishi wa Kampuni ya Uendelezaji Uwanja wa Ndege Kilimanjaro (KADCO) yanayofanyika katika ukumbi wa KADCO. Mheshimiwa Yambesi amesema ana imani mafunzo haya yataongeza tija katika usimamizi wa majukumu na utoaji wa mrejesho wa utekelezaji wa majukumu hayo kwa Taasisi na mtumishi mmoja mmoja sawa na kuongeza uelewa na hatimaye uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma katika ushughulikiaji wa haki na wajibu wa watumishi wa KADCO.

Mafunzo haya yanaratibiwa na Kitengo cha Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti (DGR) cha Tume Mada zitakazotolewa ni kuhusu Utekelezaji wa Shera ya Utumishi wa Umma Sura ya 298  na OPRAS kwa watumishi wapatao 291 wa KADCO. Wazeshaji katika mafunzo haya ni Bw. Bambumbile Mwakyanjala Mkurugenzi wa Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti, Bibi Celina Maongezi katibu Msaidizi na Bw. Fanuel Mwakibete, Afisa Kitengo cha GDR cha Tume. 

  

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.