RUFAA NA MALALAMIKO 180 YAMETOLEWA UAMUZI NA TUME
Kifungu cha 10(1) (d) na (g) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 (Marejeo ya Mwaka 2019) kimeipa Tume, Mamlaka ya kupokea na Kushughulikia Rufaa na Malalamiko ya Watumishi wa Umma mtawalia ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Mamlaka zao za Nidhamu.
Tume katika kutekeleza jukumu hili, kuanzia tarehe 27 Novemba, 2023 hadi 15 Desemba, 2023 Jijini Arusha, chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Jaji Mst. Hamisa Hamis Kalombola pamoja na Makamishna 6, ilifanya Mkutano wa pili wa mwaka 2023-2024 kupitia Rufaa na Malalamiko yaliyowasilishwa mbele yake.
Katika Mkutano huo, jumla ya Rufaa na Malalamiko 180 yaliwasilishwa na kutolewa uamuzi katika mchanganuo ufuatao:-
(i) Rufaa 155 zilisikilizwa na kutolewa uamuzi,
(ii) Malalamiko 24 yalisikilizwa na kutolewa maamuzi, na
(iii) Rufaa 1 iliahirishwa kutokana na sababu za kiufundi.