Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu

Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu

LENGO

Kutoa utaalamu na huduma za usimamizi wa rasilimaliwatu na masuala ya utawala kwa Tume. Idara hii ni Mhimili wa Uendeshaji wa shughuli za Tume za kila siku na jukumu lake la msingi ni kuhakikisha kuwa Taasisi ina nyenzo za kutosha za kufanyia kazi, nyenzo hizo ni pamoja na rasilimaliwatu, fedha, ofisi, usafiri, na samani. Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu pia ina jukumu la kusimamia utendaji kazi katika Taasisi kwa kuhakikisha kuwa malengo makuu ya Tume yanafikiwa.


Idara ina Sehemu Mbili (2);

  1. Sehemu ya Utawala; na
  2. Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu.

MAJUKUMU YA IDARA YA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU

  1. Kutafsiri Sheria ya Utumishi wa Umma, Kanuni za Utumishi wa Umma, Miongozo mbalimbali ya Utumishi wa Umma na Sheria nyingine za kazi;
  2. Kusimamia utekelezaji wa shughuli za kuhamasisha maadili kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kuzuia rushwa;
  3. Kusimamia utekelezaji wa shughuli kama vile kuajiri, uteuzi, semina elekezi, mafunzo, upandishaji vyeo, nidhamu, kuhakikisha wafanyakazi hawaondoki au kuacha kazi, motisha, kusimamia utendaji na ustawi wa wafanyakazi kwa jumla;
  4. Kuhakikisha matumizi na usimamizi wa rasilimaliwatu ulio bora na wenye ufanisi;
  5. Kuratibu masuala ya Baraza la Wafanyakazi na Vyama vya Wafanyakazi;
  6. Kusimamia uandaaji na utekelezaji wa sera, utaratibu na miongozo madhubuti ya kuajiri, mafunzo, kuhakikisha wafanyakazi hawaondoki au kuacha kazi, upandishaji vyeo na kusimamia utendaji kazi;
  7. Kuandaa Mpango wa mahitaji ya rasilimaliwatu na ujuzi unaotakiwa;
  8. Kutoa huduma za masjala na kusimamia usalama wa nyaraka na kumbukumbu za ofisi;
  9. Kuratibu masuala ya usalama wa vifaa, majengo na watumishi kazini;
  10. Kushughulikia masuala ya itifaki;
  11. Kuwezesha utoaji wa huduma za ulinzi, usafiri na mahitaji ya jumla;
  12. Kuwezesha matengenezo ya vifaa vya Ofisi, majengo na eneo la ofisi;
  13. Kuratibu utekelezaji wa masuala ya anuai; na
  14. Kuratibu utekelezaji wa Ushiriki wa Sekta Binafsi, uboreshaji wa Utendaji Kazi na Mkataba wa Huduma kwa Wateja.