Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

MKUTANO WA TUME NA.4 WA MWAKA 2019/2020 UMEHITIMISHWA LEO 04 JULAI 2020 JIJINI DAR ES SALAAM


Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, mheshimiwa Jaji (mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana, leo Jumamosi tarehe 04 Julai, 2020 amehitimisha Mkutano  wa Tume wa  kisheria namba 4 wa mwaka  2019/2020 uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 Juni 2020. Tume, katika mkutano huu  ilipokea na kutolea uamuzi Rufaa na Malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na  watumishi wa umma, ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Waajiri na Mamlaka zao za Nidhamu. Aidha, Tume  ilipokea na kujadili  taarifa mbalimbali.

Mkutano huu ulihudhuriwa na Makamishna wa Tume, waheshimiwa Bw. George D. Yambesi; Alhaji Yahya F. Mbila; Bibi Khadija A. M. Mbarak; Bibi Immaculate P. Ngwale; Balozi (Mstaafu) Daniel O. Njoolay na Balozi (Mstaafu) John M. Haule,  pamoja na Sekretarieti ya Tume.

(Taarifa zaidi kuhusu mkutano huu itatolewa..)

 

 

 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.