Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

RUFAA NA MALALAMIKO YA WATUMISHI WA UMMA YALIYOWASILISHWA TUME KUTOLEWA UAMUZI

Tume ya Utumishi wa Umma inafanya Mkutano  wake wa  Kisheria Namba 4 katika  mwaka wa fedha 2019/2020 ulioanza  leo tarehe 22 Juni, 2020  hadi tarehe 03 Julai, 2020, jijini Dar es Salaam. Katika Mkutano huu, Tume itapokea na kutolea uamuzi Rufaa na Malalamiko yaliyowasilishwa na  Watumishi mbalimbali wa Umma, ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Waajiri na Mamlaka zao za Nidhamu.

Shughuli nyingine zilizopangwa kufanyika wakati wa Mkutano huu ni pamoja na kupokea na kujadili taarifa mbalimbali. Tume inatekeleza majukumu haya kwa mujibu wa Kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298. 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.