Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

SALVATORY KAIZA, AAPISHWA KUWA KATIBU MSAIDIZI, TUME YA UTUMISHI WA UMMA

KUAPISHWA:  Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi  wa Umma, Jaji (mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana,  leo Jumanne tarehe 30 Juni, 2020 amemuapisha Bw. Salvatory Kaiza kuwa Katibu Msaidizi – Idara ya Ukaguzi na Usimamizi wa Rasilimali Watu (Sehemu ya Serikali Kuu), katika Ofisi ya Rais, Tume yaUtumishi wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti wa Tume, Jaji (mstaafu) Dkt. Bwana amemupongeza Bw. Kaiza kwa kuteuliwa  kwake na amemtakia kheri  katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Salvatory Kaiza alikuwa ni Afisa Utumishi Mkuu Daraja la Kwanza, Tume ya Utumishi wa Umma. 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.