Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Watumishi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) wapatiwa mafunzo kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298

Watumishi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ambao ni Viongozi wa Matawi ya TUGHE katika Taasisi hiyo wamepatiwa mafunzo na Bwana Salvatory Kaiza, Afisa Utumishi Mkuu (Tume ya Utumishi wa Umma) kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298. Mafunzo hayo yalitolewa katika maeneo yafuatayo:- i) Masuala ya Ajira na Marekebisho mbalimbali ya Sheria ya Utumishi wa Umma. ii) Masuala ya mchakato wa hatua za utekelezaji wa masuala ya Nidhamu kwa watumishi wa umma, na iii) Utaratibu wa kukata Rufaa kwa mtumishi ambaye hakuridhika na maamuzi ya Mamlaka yake ya Nidhamu, Utaratibu wa kukata Rufaa kwa mtumishi mtuhumiwa na Mwajiri dhidi ya Maamuzi ya Tume ya Utumishi wa Umma. Watumishi  50 wa NHIF  walishiriki mafunzo hayo.  

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.