Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

WAJIBU WA WAAJIRI, MAMLAKA ZA AJIRA NA MAMLAKA ZA NIDHAMU KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Tume ya Utumishi wa Umma inakumbusha Wajibu wa Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu katika Utumishi wa Umma, kuwa ni-

 

WAJIBU WA WAAJIRI, MAMLAKA ZA AJIRA NA MAMLAKA ZA NIDHAMU KATIKA UTUMISHI WA UMMA

1. Kusimamia na Kutekeleza kikamilifu Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayohusu masuala ya Rasilimali Watu.

2. Kuimarisha na Kuboresha Mifumo ya Utunzaji wa Kumbukumbu za kiutumishi.

3. Kuwasilisha  taarifa Tume kwa wakati na kwa kuzingatia Mwongozo wa Tume wa kuwasilisha taarifa.

4. Kuandaa Mpango wa Mafunzo unaotokana na tathmini ya mahitaji ya mafunzo na wanautekeleza.

5. Kuhakikisha Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Upimaji wa Utendaji Kazi (OPRAS) unatekelezwa ipasavyo.

6. Kusimamia na Kuzingatia kwa ukamilifu Maadili ya kazi.

7. Kuendesha Vikao vya kazi na watumishi ili kuboresha utendaji kazi wao pamoja na kujenga umoja.

 

Imetolewa na:-

 

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

6 Mtaa wa Albert Luthuli

S.L.P. 9143

Dar es Salaam

 

 

Simu: +255  (0) 738 166 703

Nukushi: +255 22 246 0 117

Barua pepe: secretary@psc.go.tz

Tovuti: www.psc.go.tz

 

 

 

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

31-05-2022

TAARIFA KWA UMMA

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.