Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe watembelea Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma-Tanzania

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe, mheshimiwa Mary Margaret Muchada na ujumbe wake walitembelea Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma iliyopo jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba 2019. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Muchada na ujumbe wake walikutana na baadhi ya Makamishna wa Tume, Mhe. George Yambesi na Mhe. Alhaj Yahya Mbila, Katibu wa Tume bwana Nyakimura Muhoji pamoja na Menejimenti ya Tume ambapo wakati wa mazungumzo waliweza kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya namna Tume ya Utumishi wa Umma inavyotekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika Kifungu cha 10 cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298.  Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe walifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi  hapa nchini hivi karibuni.  

 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.