Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Tanzia

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, ndugu Nyakimura M. Muhoji  anasikitika kutangaza kifo cha Bibi, Hafsa Anzerani Mrisho aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, “DAHRM” Tume ya Utumishi wa Umma kilichotokea usiku wa leo Jumanne tarehe 27 Machi, 2018 Dar es Salaam.

Msiba upo nyumbani kwa Baba wa marehemu Mzee Shabani Mrisho, Mwananyamala Koma Koma, Karibu na Kanisa la Anglikana. Mazishi yatafanyika leo siku ya Jumanne tarehe 27 Machi, 2018 saa 10 jioni baada ya Swala, katika makaburi ya Mwananyamala.Habari ziwafikie:-

1.   Dkt. Laurean Ndumbaro, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma akiwa Dodoma.

2.   Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana, wa Dar es Salaam.

3.   Bw. Adam Mayingu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF.

4.  Watumishi wote wa Umma, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote walipo.

 

Tume ya Utumishi wa Umma inatoa Pole kwa Familia na Wote walioguswa na Msiba Huu. “Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi – Aamiin”

“Inna Lillah wa Inna Illayhi Rajiuni”

   

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.