Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Wiki ya Utumishi wa Umma

TAARIFA KWA UMMA

KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA ITAKAYOANZA TAREHE 16 HADI 23 JUNI  2017, TUME YA UTUMISHI WA UMMA INAPENDA KUWATAARIFU WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KWA UJUMLA KUWA IMETENGA SIKU TATU (3) MAHSUSI KWA AJILI YA KUPOKEA NA KUYATOLEA UFAFANUZI MALALAMIKO  NA KERO KUTOKA KWA WADAU WAKE KUHUSU MASUALA YA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

ZOEZI LA KUKUTANA NA WADAU WA TUME LITAFANYIKA KATI YA TAREHE 16, 19 NA 20 JUNI, 2017 KUANZIA SAA 2:30 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI, KATIKA OFISI ZA TUME ZILIZOPO GHOROFA YA 7 KWENYE JENGO LA UBUNGO PLAZA, BARABARA YA MOROGORO, JIJINI DAR ES SALAAM.

AIDHA, KWA WADAU WATAKAOSHINDWA KUFIKA KATIKA OFISI ZA TUME YA UTUMISHI WA UMMA, BADO WANAYO NAFASI YA KUWASILISHA KERO AU MALALAMIKO KWA NJIA YA: 1) BARUA KWA: KATIBU, TUME YA UTUMISHI WA UMMA, S.L.P. 9143 DAR ES SALAAM. 2) BARUA PEPE: secretary@psc.go.tz.

 

“WADAU WOTE MNAKARIBISHWA”

IMETOLEWA NA:

KATIBU

TUME YA UTUMISHI WA UMMA

 

 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.