| SHEREHE ZA KUAGA WASTAAFU ZILIZOFANYIKA MWISHONI MWA MWAKA 2010 :

Wastaafu wakiwa pamoja katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika ukumbi wa
City Garden tarehe 17/12/2010. Toka kushoto ni Bibi Elly Sarakikya - aliyekuwa
Afisa Elimu Mkuu Idara ya Utumishi wa Walimu, Bibi Thecla W. Shangali
aliyekuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Samuel Ngatunga
aliyekuwa Naibu Katibu Idara ya Utumishi wa Afya na Bw. Johannes Mariki
aliyekuwa Afisa Utumishi Mkuu Idara ya Utumishi wa Serikali za Mitaa

Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo (katikati) akiteta jambo na
Mwenyekiti
wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Jovin Kitambi (kushoto)
pamoja na Kaimu Katibu wa Tume Bw. Donald Ndagula (kulia) katika hafla
ya kuwaaga wastaafu

Bw. Emmanuel Shelutete - aliyekuwa Katibu Msaidizi Idara ya Utumishi wa
Walimu akiwasilimia wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuaga wastaafu

Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo (kulia) akimkabidhi zawadi
aliyekuwa
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma
Bibi Thecla W. Shangali
(katikati) akiwa na mume wake (shoto)

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Jovin Kitambi (shoto)
akisoma hotuba ya kuwaaga wastaafu wa Tume ya Utumishi wa Umma
na
kuwapongeza
wastaafu hao kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kipindi
chao chote wakiwa watumishi wa Umma
|