Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Katibu wa Tume Bw. Nyakimura Muhoji (kulia) akifafanua kuhusu jukumu la Urekebu la Tume katika kushughulikia rufaa na malalamiko ya watumishi wa Umma. Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Tume Bw. Peleleja Masesa. M/kiti wa Tume ya Utumishi wa Umma (Jaji Mstaafu) Dk. Steven Bwana (mbele katikati) akizungumza katika kikao cha pamoja na Maafisa kutoka UNDP - Tanzania Bw. David Omozuafoh na Bi Natalie Rolloda (kulia) walipotembelea ofisi za Tume. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo kwa watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma alipotembelea ofisi za Tume na kufanya kikao na watumishi hao. Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji akizungumza na Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu katika Mkoa wa Lindi, Tume ilipofanya ziara katika mkoa huo kwa lengo la kuwajengea uwezo katika masuala ya usimamizi wa rasilimali watu. Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji akitoa neno la shukrani kwa wadau walioshiriki katika mjadala kuhusu Maadili na Haki za Binadamu uliofanyika Jijini Dodoma. Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bibi Roselyne Mboya (wa kwanza kulia) na msaidizi wake Bibi Selina Maongezi (katikati) wakitoa elimu kwa umma kupitia kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na kituo chaAzam Tv. Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Othman Chande (kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mst) George Mkuchika (Mb) wakifuatilia mjadala kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu. Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji (kulia) akifuatilia mada wakati wa mjadala kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, uliofanyika Jijini Dodoma. Washiriki wakifuatilia mada wakati wa mjadala kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa, uliofanyika Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Tume Bibi Mery Fidelis. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa  (Mb) akizungumza na watumishi wa Umma na wananchi wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya Mwl. Nyerere Square.

Karibu Tume ya Utumishi wa Umma

 

Tume ya Utumishi wa Umma imeundwa chini ya Kifungu Na. 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298. Tume ilianza kufanya kazi rasmi tarehe 7/1/2004 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua viongozi ( Mwenyekiti, Makamishna na Katibu wa Tume) kusimamia utendaji wake.

Kazi kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kusimamia uendeshaji wa shughuli za Rasilimali watu katika Taasisi za Umma na kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.

Tume ya Utumishi wa Umma inaendelea kushirikiana na wadau wake wote ili kuhakikisha kuwa U...

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.